Yohane Mbatizaji Luo Tingyin (1825 hivi - Qingyan 29 Julai 1861) alikuwa mlei wa China, mhasibu wa seminari, aliyefia Ukristo pamoja na Yosefu Zhang Wenlan, Paulo Chen Changpin na Martha Wang Luoshi.
Walifungwa katika handaki lenye joto na unyevu mwingi, waliteswa kikatili na hatimaye walikatwa kichwa[1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].