Yohane Kinuya alikuwa Mkristo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko aliyefia dini nchini Japani (1597).
Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[1]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu [2].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[3].