Pekupeku (kwa Kiingereza: Discalced) ni jina linalotumika kuhusu watu wanaotembea bila viatu.
Limetumika rasmi kwa ajili ya mashirika ya kitawa au matawi yake yaliyoelekeza wanajumuia kutembea hivyo katika juhudi kwa ajili ya ufukara wa hiari, kama waliofanya Fransisko wa Asizi na Klara wa Asizi katika Italia ya karne ya 13.
Maarufu zaidi ni Ndugu Wadogo Pekupeku wa Petro wa Alkantara na Wakarmeli Peku wa Teresa wa Yesu na Yohane wa Msalaba katika Hispania ya karne ya 16.