Uwanja wa michezo wa Jeshi la Misri (Kiar. ستاد الجيش المصري بالسويس sitad al-jaish al-masri bil-suwais) ni uwanja wa Jeshi la Misri huko Suez. Ni uwanja unaotumika na mashirika ya mchezo wa mpira wa miguu huko Suez, nchini Misri. Uwanja huo ulijengwa mnamo mwaka 2009 ukawa kama moja ya viwanja vilivyotumika kwa mkutano wa Kombe la Dunia FIFA mwaka 2009, ambalo wenyeji walikuwa ni Misri.[1]
Uwanja huo ulijulikana kama Uwanja wa Kimataifa wa Mubarak hadi mwaka 2011 na ulibadilishwa kuwa Uwanja wa Jeshi la Misri kama matokeo ya mapinduzi ya Misri ya mwaka 2011, ambayo yalimuondoa Hosni Mubarak kutoka kuwa urais wa Misri.[2] [3][4]
{{cite web}}
|archivedate=
|archive-date=
|archiveurl=
|archive-url=
|=
|https://www.webcitation.org/6HnkIkcbx?url=