Katika vita zilizofuata Waingereza walifaulu kutokana na matumizi ya teknolojia ya silaha iliyoendelea na baada ya vita ya tano kati ya Uingereza na Ashanti ufalme wote ulikuwa sehemu ya koloni la Gold Coast tangu 1 Januari1902.
Leo, Ufalme wa Ashanti umebaki kama sehemu ya Jamhuri ya Ghana. Unatambuliwa kama "mamlaka ya kimila" ukitajwa vile katika katiba ya Ghana. [6]
Mfalme wa sasa ni Otumfuo Osei Tutu II Asantehene. Ziwa Bosumtwi ambalo ni ziwa asilia pekee ya Ghana liko ndani ya ufalme. [7]
Maeneo ndani ya Ashanti yalikuwa na dhahabu kutoka mito, kakao na mikola. Waashanti walitumia bidhaa hizo katika biashara yao na Wareno kwenye pwani, na milki jirani za Songhai na Wahausa.[9]
Utumwa
Utumwa ulikuwa sehemu ya utamaduni katika Ufalme wa Ashanti. Kwa kawaida watumwa walipatikana kama mateka kutoka kwa maadui katika vita. Ashanti ilikuwa dola lenye watumwa wengi katika eneo la Ghana ya leo, ilikuwa pia chanzo kikuu cha watumwa kwa biashara ya watumwa ya Atlantiki.[10]
Kimila ustawi wa watumwa ulitegemea hali ya mabwana wao. Wengine waliweza kuwa na mali ya binafsi, na hata kuoa au kuolewa katika familia ya bwana wao. Watumwa wakati mwingine waliweza kumiliki watumwa wengine, na pia kuomba bwana mpya ikiwa waliamini kuwa wananyanyaswa sana. [11] Lakini ilikuwa pia kawaida kuwatoa kama dhabihu wakati wa mazishi ya bwana.
Mateka waliokamatwa kwa kusudi la kuwauza kwa wafanyabiashara Wazungu kwenye vituo vya pwani walitendewa kama bidhaa.
↑Green, Toby. A fistful of shells : West Africa from the rise of the slave trade to the age of revolution (tol. la Penguin Books Ltd. Kindle-Version). London. ku. 108, 247. ISBN978-0-241-00328-2.
↑Shumway, Rebecca. The Fante and the transatlantic slave trade. Rochester, NY. uk. 237. ISBN978-1-78204-572-4.
↑Roeder, Philip (2007). Where Nation-States Come From: Institutional Change in the Age of Nationalism. Princeton: Princeton University Press. uk. 281. ISBN978-0691134673.