Paulo, Sirili na wenzao walikuwa Wakristo wa Antiokia ya Syria (leo nchini Uturuki) waliofia imani yao.
Kati ya wenzao wanatajwa Eujeni, Serapioni, Tigrini, Klaudi, Esuperi, Viktorisi, Valentini na Domni, lakini hakuna hakika juu yao[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 20 Machi[2].