Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote. Ona namna ya kutaja vyanzo hapa: Wikipedia:Umaarufu na Kutaja vyanzo. Ni lazima kuboresha makala kwa kutafuta vyanzo na kuvitaja kama marejeo, la sivyo sehemu ya makala au yote kabisa inaweza ikafutwa. Unaweza kuondoa kigezo hiki mara baada ya vyanzo sahihi kuwa vimeingizwa katika makala
Katika jiografia, Oasisi ni eneo lenye mimea katikati ya jangwa, kwa kawaida likizunguka chemchemi au chanzo kingine cha maji. Oasisi pia hutoa makazi kwa wanyama na hata binadamu kama eneo ni kubwa vya kutosha.
Maeneo yenye oasisi yamekuwa muhimu kwa biashara na njia za usafiri katika maeneo ya jangwa. Misafara hulazimika kupitia karibu na oasisi ili kujiongezea akiba zao za maji na chakula. Hivyo, kudhibiti kisiasa au kijeshi Oasisi mara nyingi kunamaanisha kudhibiti biashara ya misafara fulani. Kwa mfano, oasisi za Awjila, Ghadames na Kufra iliyoko katika Libya ya leo, kwa nyakati mbalimbali zimekuwa muhimu kwa biashara za Kaskazini-Kusini na Mashariki-Magharibi katika biashara ya ng'ambo ya Sahara.
NenoOasisi liliingia katika Kiingereza kutoka neno la Kigirikiὄασις Oasis, lililotoholewa moja kwa moja kutoka neno la Misriwḥ3t au Demoticwḥỉ.
Oasisi hutokana na mito iliyo chini ya ardhi au aquifer kama vile artesian aquifer, ambapo maji yanaweza kufikia juu kwa shinikizo la kimaumbile au kwa watu kuchimba visima. Gharika fupi za mara kwa mara hutoa maji chini ya ardhi na kuendeleza oasisi, kama vile Tuat. Miamba na mawe iliyo chini ya ardhi na isiyopenyeza maji inaweza kuyateka maji na kuyahifadhi katika mifuko; au katika sehemu ndefu chini ya ardhi zenye maeneo hafifu au mitaro ya volkeno maji yanaweza kukusanyika na kububujika juu ya ardhi. Matukio yoyote ya maji hutumiwa na ndege wakihama na pia kupitisha mbegu pamoja na mavi yao ambazo hukua kandokando ya maji hayo na kutengeneza Oasisi.
Kupanda mimea
Watu wanaoishi katika Oasisi hawana budi kusimamia kwa makini matumizi ya ardhi na maji; mashamba lazima yanyunyiziwe maji ili kukuza mimea kama vile mitende, mitini, mizeituni na miaprikoti. Mmea muhimu zaidi katika Oasisi ni mitende ambao hutengeneza safu ya juu. Mitende hiyo hutoa kivuli kwa miti midogo kama vile ya Peach, ambayo huwa katika safu ya katikati. Kwa kupanda mimea katika matabaka mbalimbali, wakulima hutumia ardhi na maji bora zaidi. Mboga nyingi pia hukuzwa na baadhi ya nafaka, kama vile ngano, shayiri na mtama hukuzwa katika maeneo yenye unyevu zaidi.
[1]
Oasisi maarufu
Afrika
Bonde la Mto Nile na delta, Misri, linadaiwa kuwa Oasisi kubwa zaidi ulimwenguni kote katika toleo la 2007 la Guinness Book of World Records likiwa na eneo lenye kilomita mraba 22,000.
Bonde la Las Vegas Valley, Marekani, lililokuwa Oasisi limekuwa jangwa la Mojave na katika miaka iliyopita limekua na kuwa eneo lenye zaidi ya watu milioni 1.8, eneo maarufu kwa Las Vegas Strip
(Kifaransa) Marejeo: Jardins au Desert (Vincent Battesti) | Battesti (Vincent), Jardins au desert, Evolution des pratiques et savoirs oasiens, Jérid tunisien, Paris, Editions IRD, coll. À travers champs, 2005, 440 p. ISBN 2-7099-1564-2Open Archives: book in free access / in French