Mipango ilianza baada ya wazo hilo kuchukuliwa na serikali ya Marekanimwaka1984, mradi huo ulizinduliwa rasmi mnamo 1990, na ulitangazwa kuwa kamili mnamo Aprili 14, 2003.[3] Kiwango cha jenomu kamili kilifanikiwa mnamo Mei 2021. [4][5]
Mradi wa Jenomu ya Binadamu hapo awali ulilenga kutengeneza ramani ya nyukleotidi zilizomo kwenye jenomu ya rejeleo lenye seti moja ya chembeuzi za binadamu (zilizo zaidi ya bilioni tatu). Jenomu ya kila mtu ni ya pekee; kupanga ramani ya jenomu ya binadamu kulihusisha kutafiti mlolongo wa ADN katika idadi ndogo ya watu na kisha kukusanya taarifa hizo ili kupata mlolongo kamili kwa kila chembeuzi. Kwa hiyo, jenomu ya binadamu iliyomalizika ni mozaiki kwa sababu ina mchanganyiko wa taarifa za seli kutoka kwa zaidi ya mtu mmoja, haimwakilishi mtu yeyote maalumu. Manufaa ya mradi huo yanatokana na ukweli kwamba sehemu kubwa ya jenomu ya binadamu ni sawa kwa wote.