Koskoni, Zenoni na Melanipo (walifariki Nisea, Bitinia, leo nchini Uturuki, karne ya 3) walikuwa Wakristo waliofia dini yao hiyo wakati wa dhuluma ya Dola la Roma[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 18 Januari[2].