Herodoti ni maarufu kwa sababu alikusanya habari nyingi za historia ya kale ya mataifa ya Asia, Afrika na Ulaya. Waroma wa Kale walimwona kama "Baba wa historia".
Sehemu kubwa ya maandishi yake yamepotea; yanajulikana tu kwa sababu yanatajwa katika vitabu vingine vya kale. Lakini historia yake ya vita kati ya Wagiriki na Wajemi wakati wa karne ya 5 na 6 KK imehifadhiwa.
Kwa jumla hata wataalamu wa leo hutegemea mara nyingi habari zilizokusanywa na Herodoti juu ya Babeli, Misri, Uajemi na Ugiriki ya Kale.
Vyanzo
The History of Herodotus, jinsi ilivyotafsiriwa na George Rawlinson kwa Kiingereza, Vitabu 1 - 9, (1860)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Herodoti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.