Epimako, Aleksanda na wenzao Merkuria, Dionisya, Amonaria na mwanamke mwingine (walifia dini Aleksandria, Misri, 12 Desemba 250 hivi) walikuwa Wakristo ambao waliuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[1].
Wanaume, baada ya kufungwa muda mrefu na kuteswa kwa namna mbalimbali, hatimaye walichomwa moto wakiwa hai kwa sababu ya kumuamini Yesu Kristo.
Kumbe wenzao walikatwa kichwa mara moja kwa kuwa hakimu aliogopa kutiwa aibu ikiwa wanawake watamshinda kwa kuvumilia kwa uimara mateso ya kila aina [2].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini, na Amonaria kama bikira pia.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Desemba[3][4].