Digamma (kigiriki δίγαμμα ikaandikwa kama Ϝ au ϝ) ilikuwa kiasili herufi ya sita ya alfabeti ya Kigiriki. Sauti yake ilikuwa kama V au F. Asili yake ilikuwa Waw ya Kifinisia.
Baadaye ilifutwa katika alfabeti ya Kigiriki kwa sababu lugha ilipoteza sauti hiyo. Alama ilitumiwa kwa namba 6 pekee.
Lakini Waetruski walifufusha alama wakaihitaji kwa sauti ya F ikaingia hivyo katika alfabeti ya Kilatini na kuendelea vile.
Viungo vya Nje