Basili, Eujeni na wenzao Agatodoro, Elpidi, Eteri, Kapitoni na Efremu (walifariki Kersoneso, leo nchini Ugiriki, mwishoni mwa karne ya 3 - mwanzoni mwa karne ya 4) walikuwa maaskofu wamisionari kutoka Yerusalemu ambao waliuawa kwa sababu ya imani yao, isipokuwa labda Kapitoni[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 7 Machi[2].