Kufuatana na taarifa za Injili ya Luka (11:2-4) maneno ya sala hii yalitolewa na Yesu Kristo alipoombwa na wanafunzi wake awafundishe jinsi ya kusali baada ya wao kutambua kidogo anavyosali vizuri.
Toleo la Luka ni fupi zaidi, likiwa na maombi 5 tu badala ya 7.
Tafsiri za Kiswahili
Kwa Kiswahili kuna maumbo tofauti kwa sababu sala ilitafsiriwa na wamisionari mahali mbalimbali kwa wakati tofauti na kuwa kawaida kimahali. Haikusanifishwa hadi leo kwa Wakristo wote wanaotumia Kiswahili. Maumbo mawili yanayotumiwa zaidi ni kama ifuatavyo:
BABA YETU mtakatifu kabisa:
muumba, mkombozi, mfariji na mwokozi wetu.
ULIYE MBINGUNI: katika malaika na katika watakatifu,
ukiwaangazia wawe na ufahamu, kwa sababu wewe Bwana ni mwanga;
ukiwawasha wawe na upendo, kwa sababu wewe Bwana ni upendo;
ukikaa ndani mwao na kuwajaza furaha, kwa sababu wewe Bwana
ni wema mkuu kabisa, wema wa milele,
ambaye kwako hutoka mema yote, na bila yako hakuna jema.
JINA LAKO LITUKUZWE: ujuzi wetu juu yako uwe wazi zaidi na zaidi,
tuweze kujua upana wa baraka zako, urefu wa ahadi zako,
kimo cha ukuu wako, kina cha hukumu zako.
UFALME WAKO UFIKE: utawale ndani yetu kwa njia ya neema yako
na kutuwezesha kuingia katika ufalme wako ambapo
unaonekana kama ulivyo, unapendwa kikamilifu,
unatia heri ya kukaa nawe, unatia raha ya kukufurahia milele.
UTAKALO LIFANYIKE DUNIANI KAMA MBINGUNI: tuweze kukupenda
kwa moyo wetu wote, kwa kukuwaza wewe daima;
kwa roho yetu yote, kwa kukutamani wewe daima;
kwa akili yetu yote, kwa kuelekeza nia zetu zote kwako
na kwa kutafuta utukufu wako katika yote;
kwa nguvu zetu zote pia, kwa kutumia uwezo na hisia zote
za roho na mwili katika kuhudumia upendo wako na si chochote kingine;
na tuweze kuwapenda majirani wetu kama tunavyojipenda,
kwa kuwavuta wote kwa nguvu zetu zote kwenye upendo wako,
tukifurahia mema ya wengine kama tunavyofurahia ya kwetu,
na tukihuzunika pamoja na wengine kwa mabaya yanayowafikia,
bila ya kumuudhi yeyote.
MKATE WETU WA KILA SIKU: Mwanao mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo.
UTUPE LEO: kwa ukumbusho, ufahamu na heshima
ya upendo ule aliokuwanao kwetu sisi
na ya mambo yale ambayo alisema na kutenda na kuteseka kwa ajili yetu.
UTUSAMEHE MAKOSA YETU: kwa huruma yako isiyosemeka,
kwa nguvu ya mateso ya Mwanao mpendwa,
pamoja na stahili na maombezi ya Bikira mbarikiwa daima
na ya wateule wako wote.
KAMA TUNAVYOWASAMEHE NA SISI WALIOTUKOSEA:
na lolote tusilosamehe kikamilifu,
wewe Bwana utuwezeshe kulisamehe kabisa,
tuwapende kweli maadui wetu kwa ajili yako,
na tuwaombee kwa bidii mbele zako, bila ya kumlipa yeyote ovu kwa ovu,
bali tukijitahidi kumsaidia kila mmoja katika wewe.
NA USITUTIE KATIKA VISHAWISHI: kilichofichika au cha wazi,
cha ghafla au cha muda mrefu.
LAKINI UTUOPOE MAOVUNI: yaliyopita, ya sasa na yajayo.
ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU
KAMA MWANZO, NA SASA NA MILELE. AMINA.
Mengineyo
Baba Yetu kwa lugha nyingi
Katika "Bustani ya ufufuo" (Resurrection Gardens) mjiniNairobi, mtaa wa Karen, kuna maonyesho ya tafsiri ya Baba Yetu katika lugha mamia. Maneno yamechongwa na wasanii katika mawe, katika ubao au kuchorwa kwenye vigae. Hii inafuata mfano wa kanisa la Paternoster mjini Yerusalemu lenye tafsiri za Baba Yetu kwa lugha 140 kwenye vigae vya rangi (tazama Viungo vya Nje hapo chini).
Wimbo ni wa kuvutia lakini kwa bahati mbaya maneno ya sala yamefupishwa kwa namna inayodokeza kwamba mhariri aliyepanga maneno kwa tuni na pia waimbaji hawakuelewa Kiswahili.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Baba yetu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!