Mwaka711Waarabu na Waberber Waislamu walivamia Hispania kwa kuvuka mlango wa Gibraltar na kuanzisha utawala wao katika sehemu kubwa za rasi ya Iberia uliokwisha mwaka 1492. Kati ya maeneo yote ya Hispania ni Andalusia iliyokaa muda mrefu chini ya utawala wa Kiislamu. Eneo lote chini ya utawala wa Kiislamu likaitwa "Al-Andalus" na Andalusia ya leo ilikuwa kiini chake.
Kati ya mabaki ya kipindi hicho ni majengo kama Alhambra wa Granada, majina ya kijiografia kama mto Guadalquivir (kutoka Kiarabuالوادي الكبير "wadi al kabir" yaani mto mkubwa) na muziki wa Andalusia.
Utawala
Jimbo la Andalusia huwa na mikoa 8. Mahakama hufanya kazi kwenye msingi wa maeneo ya korti kwa jumla ni 125 katika Andalusia.
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Andalusia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.