Alois na Maria Azelia Martin walikuwa mume na mke wa Ufaransa katika karne ya 19 BK[1].
Ni maarufu kutokana na maandishi ya mwanao wa tisa na wa mwisho, Teresa wa Mtoto Yesu.
Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu. Papa Benedikto XVI aliwatangaza wenye heri tarehe 19 Oktoba 2008, halafu Papa Fransisko watakatifu tarehe 18 Oktoba 2015.
Sikukuu yao inawaadhimisha kwa pamoja tarehe 12 Julai[2].
Mwaka 2011, barua zao[3] zilichapishwa kwa Kiingereza kwa jina la A Call to a Deeper Love: The Family Correspondence of the Parents of Saint Therese of the Child Jesus, 1863–1885 (ISBN 0818913215).