Yohane Houghton

Mt. Yohane alivyochorwa na Francisco Zurbarán.

Yohane Houghton, O.Cart. (Essex[1], 1487 hivi – Tyburn, 4 Mei 1535) alikuwa padri wa Uingereza, priori wa monasteri ya Wakartusi ya London[2] na mkuu wa shirika hilo nchini.

Kwa kukiri imani ya mababu na kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme Henri VIII kama mkuu wa Kanisa Uingereza badala ya Papa alinyongwa ila kabla hajafa alikatwa vipandevipande ambayo vilitundikwa sehemu mbalimbali za mji[3]. Pamoja naye waliuawa mapriori wawili wengine wa shirika hilo, Robati Lawrence na Augustino Webster, tena padri Richard Reynolds wa shirika la Mt. Birgita na paroko mwanajimbo Yohane Haile.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 9 Desemba 1886 na mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970 na Papa Paulo VI.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake[4].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!