William Nicholaus Lyimo (maarufu kwa jina la kisanii Bill Nass [1] [2] [3]; amezaliwa 11 Aprili 1993) ni rapa wa Kitanzania. MTV Base ilimtaja kati ya "Wasanii 50 walio tazamwa Kwa Mwaka 2017". [4] Miezi kadhaa baada ya kutolewa kwa wimbo wake wa kwanza "Raha", [5]
Bill Nass aliteuliwa kuwania Tuzo za Muziki za Kilimanjaro Tanzania (KTMA) za mwaka 2015 kama "Msanii Mpya Bora". [6] [7]
Bill Nass ameshinda tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume wa Hip hop Mwaka 2022.