Walter von Saint Paul-Illaire

St. Paul-Illaire

Walter von Saint Paul-Illaire au Adalbert Emil Walter Le Tanneux von Saint Paul-Illaire (Berlin, Januari 12, 1860 - Berlin, Desemba 12, 1940) alikuwa ofisa wa wilaya ya koloni la Ujerumani katika Afrika Mashariki (Afrika Mashariki ya Kijerumani).

Familia yake, Le Tanneux von Saint Paul, ilikuwa ya kisharifu kutoka zamani sana, na ilihamia Prussia katika karne ya 17. [1]

Maua ya aina ya 'viola' au 'violet' (kwa Kiajemi: بنفسج) katika jenasi Saintpaulia, yalipewa jina lake baada ya kuonekana katika matembezi yake ya Milima ya Usambara mwaka wa 1893. Alituma mbegu ya maua hayo kwa Hermann Wendland, mtaalamu wa botania wa Ujerumani, na Mkuu wa bustani ya Kifalme, bustani za Herrenhausen huko Hannover. Huyo alitoa habari ya kwanza ya mimea hiyo, na aliita mimea hii Usambara veilchen ('Violeti ya Usambara'). [2] [3]

Maisha

Baba wa Walter von Saint Paul-Illaire, Ulrich von Saint Paul-Illaire (1833-1902), alikuwa ofisa katika jeshi la wanamaji na mwanachama wa Dola la Ujerumani (kwa Kijerumani: Deutsches Reich). Baba yake alipendezwa sana na miti, hasa miti ya misunobari, na alimwuliza kwa barua na George Engelmann, daktari na mwanabotania wa Missouri, maelezo ya anzisho na uwezo wa kutumia miti kati ya misunobari inayoitwa Engelmann spruce. Labda upendo wake wa botania ulimtia mtoto wake, Walter, hamu ya kun'gamua mimea.[4] [5] .

Mnamo 1885, Walter von Saint Paul-Illaire alikuwa mshiriki wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki(Kijerumani: Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft(DOAG)). Januari 1886, yeye alsafiri nchini Kenya ya leo.[6] Baadaye, mwaka wa 1889, alikua mkurugenzi wa forodha na wakala mkuu wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki huko Zanzibar(Unguja). Mnamo 1891, Dola la Ujerumani (Kijerumani: Deutsches Reich) lilishika usimamizi wa Afrika Mashariki ya Ujerumani. St. Paul-Illaire alianza kufanya kazi ya ofisa ya wilaya ya Tanga kutoka 1891 mpaka 1900.[7] Wakati huu alipenda kutembea katika milima na miamba ya Usambara, karibu na Tanga, na alifurahi sana kuona mimea hii, pamoja na rangi ya samawati ya maua yake. Jina la spishi, ionantha, limetokana na Kigiriki, 'ίον', kwa ajili ya rangi ya zambarau, na 'άνθος', ambayo inamaanisha maua.[8]Siku hizi mmea huu umejumuishwa ndani ya jenasi ya Streptocarpus.[9]

Saintpaulia ionantha

Katika jukumu lake la ukoloni, alishughulika katika masuala ya kazi katika koloni ya Afrika Mashariki ya Ujerumani,[10] na pia alitoa hoja kuondoa na kuwatenga Wahindi wa koloni kwa sababu walikuwa idadi kubwa ya watu wa rangi waliofanya biashara ya rejareja na Waafrika, na kwa wengi, alibishi walitumia vitabu vya hesabu bila kufuata kawaida ya Ulaya.[11] Saint Paul-Illaire alikuwa pia mwandishi wa kikoloni wa gazeti la Cologne, Kölnische Zeitung, na mwaka wa 1896 alichapisha kamusi ya Kiswahili. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, katika hotuba chini ya jina la "Africanus", aliomba wajumbe wa Amerika na wa Britania kwenye Mkutano wakuleta Amani(1919-1920), huko Paris, warudishe makoloni ya Ujerumani.[12] [13]

Kifo

Alifariki huko Berlin mnamo 1940, akazikwa katika makaburi ya Invalidenfriedhof kulekule, lakini kaburi lake halijahifadhiwa. [14] "Aligundua" mimea ya maua ya 'violeti ya Kiafrika' yeye, lakini ilikuwa mashuhuru duniani, kama mimea ya vyungu, baada ya kifo chake.

Machapisho

  • Swahili-Sprachführer. Daresalaam 1896. [15]
  • Kriegs-Xenien: Stimmen und Stimmungen aus dem Weltkriege. Leipzig 1919.
  • Der Fluch der deutschen „Gewissenhaftigkeit“. Berlin 1921.

Marejeo

  1. Genealogisches Handbuch des Adels, Adelslexikon Band XIV, Band 131 der Gesamtreihe, C. A. Starke Verlag, Limburg (Lahn) 2003, ISSN 0435-2408, S- 319–320
  2. Eastwood, A., et al. “THE CONSERVATION STATUS OF SAINTPAULIA.” Curtis's Botanical Magazine, vol. 15, no. 1, 1998, pp. 49–62. JSTOR, www.jstor.org/stable/45065280. Accessed 4 June 2021.
  3. "Early Discovery and Naming | Gesneriad Reference Web".
  4. "Correspondence Saint Paul-Illaire (Ulrich) and Engelmann (George)" https://ia600500.us.archive.org/16/items/mobot31753004062557/mobot31753004062557.pdf
  5. "Picea engelmannii (Engelmann spruce) description".
  6. Wie Deutsch-Ostafrika entstand : mit dem Bildnis des Verfassers und einer Karte / von Dr. Carl Peters Liepzig 1912. http://lbsopac.rz.uni-frankfurt.de/CMD?ACT=SRCHA&IKT=6015&DB=30&TRM=ppn:402491491
  7. Ulrich van der Heyden: Koloniales Gedenken im Blumentopf: Das Usambara-Veilchen und sein „Entdecker“ aus Berlin, in: Ulrich van der Heyden und Joachim Zeller (Hrsg.): Kolonialismus hierzulande – Eine Spurensuche in Deutschland. Sutton Verlag, Erfurt 2007, ISBN 978-3-86680-269-8, S. 220–222.
  8. "Origins of African Violets and Impatiens". pss.uvm.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-11. Iliwekwa mnamo 2021-07-27.
  9. "The Great Merger – Current Taxonomic Status | Gesneriad Reference Web".
  10. Die Arbeiterfrage in Deutsch-Ostafrika; W. von St. Paul Illaire: Deutsche Kolonialzeitung › 26 (1909) › 4 (23.1.1909) p57 - 59 https://sammlungen.ub.uni-frankfurt.de/kolonialbibliothek/periodical/pageview/7864168?query=illaire
  11. Zur Indierfrage in Deutsch-Ostafrika; WaIter v. St. Paul-Illaire: Jahrbuch Uber die deutschen Kolonien, Jahrg. 3 (1910) p. 254-263 https://brema.suub.uni-bremen.de/dsdk/periodical/titleinfo/1996560
  12. "The adjustment of the German colonial claims; dedicated to the American and British delegates of the Peace conference" https://archive.org/details/adjustmentofgerm00afririch/page/n1/mode/2up
  13. Deutsche Bücherei (Leipzig): Weltkriegssammlung Erscheinungsdatum: 1918 http://d-nb.info/576354082
  14. "Walter of Saint Paul-Illaire - ZXC.wiki".
  15. "Kolonialbibliothek / Swahili-Sprachführer".

Read other articles:

Taksinyang Agung สมเด็จพระเจ้าตากสินมหาราชRaja Borommaracha IVPatung Raja Taksin di Istana Hat-Sung (Wat Khung Taphao, Provinsi Uttaradit, Thailand)Raja ThonburiBerkuasa28 Desember 1767 – Maret 1782Penobatan28 Desember 1767PendahuluEkkathat dari Ayutthaya (sebagai Raja AyutthayaPenerusBuddha Yodfa Chulaloke dari Rattanakosin (Rama I) (sebagai raja Rattanakosin)WaliInthraphithakInformasi pribadiKelahiran(1734-04-17)17 April 1734Ayutthaya, Ker...

 

هذه المقالة يتيمة إذ تصل إليها مقالات أخرى قليلة جدًا. فضلًا، ساعد بإضافة وصلة إليها في مقالات متعلقة بها. (أبريل 2019) جوشوا ليون معلومات شخصية الميلاد 25 يونيو 1974 (49 سنة)  مواطنة الولايات المتحدة  الحياة العملية المدرسة الأم الجامعة الحكومية في نيويورك في بيرتشايس  ال...

 

O Bodião de cabeça azul ou Gudião azul (Thalassoma bifasciatum)[1], é uma espécie de Bodião da família Labridae, do gênero Thalassoma. Bodião de cabeça azul Thalassoma bifasciatum Estado de conservação Quase ameaçada Classificação científica Reino: Animalia Filo: Chordata Classe: Actinopterygii Ordem: Perciformes Família: Labridae Género: Thalassoma Espécie: T.bifasciatum Nome binomial 'Thalassoma bifasciatum'Bloch, 1791 Habitat São encontrados em recifes de corais costeir...

هذه المقالة يتيمة إذ تصل إليها مقالات أخرى قليلة جدًا. فضلًا، ساعد بإضافة وصلة إليها في مقالات متعلقة بها. (يناير 2019) يصف نموذج بابكوك آلية يمكن أن تفسر الأنماط المغناطيسية والبقع الشمسية الملاحظة على الشمس. التاريخ يبدأ الفهم الحديث للبقع الشمسية مع جورج هيل، الذي ربط المجا

 

American novelist This article needs additional citations for verification. Please help improve this article by adding citations to reliable sources. Unsourced material may be challenged and removed.Find sources: Paul W. Fairman – news · newspapers · books · scholar · JSTOR (September 2018) (Learn how and when to remove this template message) Paul W. Fairman c.1956 Paul Warren Fairman (1909–1977) was an editor and writer in a variety of genres under ...

 

Cet article est une ébauche concernant une station de métro et le Japon. Vous pouvez partager vos connaissances en l’améliorant (comment ?) selon les recommandations des projets correspondants. Sekime-Takadono Vue de la station Localisation Pays Japon Ville Osaka Arrondissement Asahi Adresse 4 Takadono, Asahi-ku, Ōsaka-shi Coordonnéesgéographiques 34° 42′ 55″ nord, 135° 32′ 45″ est Géolocalisation sur la carte : préfecture d'Osaka Ca...

Institut Ilmu Kesehatan Bhakti WiyataIIK Bhakta : Institut Kesehatan Pertama di Indonesia[1]Nama sebelumnyaPendidikan Bhakti Husada 1985MotoDeveloping Health ExpertsMoto dalam bahasa IndonesiaMengembangkan Ahli KesehatanMoto dalam bahasa InggrisDeveloping Health ExpertsDidirikan2005 (2005)[2]PendiriDr. Bambang Harsono Suhartono, MBA.AfiliasiYayasan Bhakti WiyataAfiliasi akademikKemenristek Dikti RI, Kemenkes RIAkreditasiBRektorProf. Dr. Muhamad Zainuddin, A...

 

Overview of the legality and prevalence of abortions in the U.S. state of Missouri This article may need to be rewritten to comply with Wikipedia's quality standards. You can help. The talk page may contain suggestions. (June 2020) Abortion in Missouri is illegal, with abortions only being legal in cases of medical emergency and several additional laws making access to abortion services difficult.[1] In 2014, a poll by the Pew Research Center found that 52% of Missouri adults said tha...

 

2004 studio album by Matthew Good White Light Rock & Roll ReviewStudio album by Matthew GoodReleasedJune 15, 2004RecordedMushroom Studios and Warehouse Studios, Vancouver, British Columbia, CanadaGenreRockLength48:43LabelUniversal Music CanadaProducerWarne LiveseyMatthew Good chronology Avalanche(2003) White Light Rock & Roll Review(2004) In a Coma:1995-2005(2005) Singles from White Light Rock & Roll Review Alert Status RedReleased: 2004 In Love With A Bad Idea / It's Been A W...

Не следует путать с Герреро. Гереро Численность 200 тыс. чел Расселение  Намибия  Ботсвана  Ангола Язык гереро, африкаанс, английский, португальский, Религия Протестантизм, традиционные верования Родственные народы народы банту  Медиафайлы на Викискладе Группа ...

 

此條目没有列出任何参考或来源。 (2013年6月22日)維基百科所有的內容都應該可供查證。请协助補充可靠来源以改善这篇条目。无法查证的內容可能會因為異議提出而被移除。 侯俊傑(1961年9月28日—),筆名侯捷,台灣電腦技術專欄作家,致力於電腦技術之紮根工作,文章兼具科技之長與靈性之美[1],有讀者的評語是「比作家更工程師,比工程師更作家」。大同國中、...

 

Annual race in Australia held since 1979 Gold Coast MarathonStarting line of the 1986 raceDateJulyLocationGold Coast, Queensland, AustraliaEvent typeRoadDistanceMarathon, half marathonPrimary sponsorChery MotorEstablished1979 (44 years ago) (1979)Course recordsMen's: 2:07:50 (2019) Yuta ShitaraWomen's: 2:24:43 (2022) Lindsay FlanaganOfficial siteGold Coast MarathonParticipants5,769 (2019) The Gold Coast Marathon is an annual road marathon on the Gold Coast, Queensland, Australia...

Former art gallery in Los Angeles, United States Sonos StudioEstablishedMay 9, 2012; 11 years ago (2012-05-09)LocationLos AngelesTypeArt galleryStudioOwnerSonosWebsitehttps://www.sonos.com/ Sonos Studio is an art gallery and studio in Los Angeles, United States, established on May 9, 2012, and owned by American consumer electronics company Sonos. The studio has also had temporary pop-up locations in New York City, London, and Amsterdam. In 2016, the Los Angeles studio perman...

 

Former proglacial lake in New Jersey, U.S. This article needs additional citations for verification. Please help improve this article by adding citations to reliable sources. Unsourced material may be challenged and removed.Find sources: Lake Passaic – news · newspapers · books · scholar · JSTOR (July 2022) (Learn how and when to remove this template message) Approximation of the extent of Glacial Lake Passaic Lake Passaic was a prehistoric proglacial ...

 

Albanian singer (born 1998) Arilena AraAra at the 58th edition of Festivali i KëngësBorn (1998-07-17) 17 July 1998 (age 25)Shkodër, AlbaniaOccupation(s)Singer, television presenterYears active2010 – presentWebsitearilenaara.com Arilena Ara (Albanian: [aɾiˈlɛna ˈaɾa]; born 17 July 1998) is an Albanian singer and television presenter. Ara rose to national recognition in Albania, upon her victory at X Factor Albania in 2013. After her participation in the...

Voor het meten van zeegolven zijn verschillende methoden ontwikkeld. Het probleem bij het meten van zeegolven is het stochastische gedrag en de omgeving die vaak tot schade aan instrumenten leidt. Een natuurlijk golfveld met zeegolven bestaat uit golven van verschillende hoogten. Om de maatgevende hoogte van dit golfveld vast te leggen is de significante golfhoogte ingevoerd. Deze wordt aangegeven met het symbool Hs. In het verleden was dit de golfhoogte die visueel geschat werd door een getr...

 

Battle in the American Civil War Battle of White Oak SwampPart of the American Civil WarBattle at White Oak Swamp BridgeAlfred R. Waud, artist, June 1862DateJune 30, 1862 (1862-06-30)LocationHenrico County, Virginia37°28′15″N 77°12′37″W / 37.4708°N 77.21025°W / 37.4708; -77.21025Result InconclusiveBelligerents United States (Union) CSA (Confederacy)Commanders and leaders William B. Franklin Thomas J. Stonewall JacksonUnits involved Units from...

 

Being killed by the falling fruit Bilingual warning sign in Honolulu, written in English and Japanese Coconuts falling from their trees and striking individuals can cause serious injury to the back, neck, shoulders and head, and are occasionally fatal.[1] Following a 1984 study on Injuries Due to Falling Coconuts, exaggerated claims spread concerning the number of deaths by falling coconuts. Falling coconuts, according to urban legend, kill a few people a year. This legend gained mome...

هذه المقالة بحاجة لصندوق معلومات. فضلًا ساعد في تحسين هذه المقالة بإضافة صندوق معلومات مخصص إليها. حد توف أو حد كتلة توف في الفلك (بالإنجليزية : Tolman-Oppenheimer-Volkoff-Grenze أو TOV) هي أكبر كتلة لنجم يتكون من مادة نيوترونية منفطرة تنتج نجما نيوترونيا. وهي تماثل حد كتلة شاندراسيخار الت...

 

此條目可参照英語維基百科相應條目来扩充。 (2022年3月22日)若您熟悉来源语言和主题,请协助参考外语维基百科扩充条目。请勿直接提交机械翻译,也不要翻译不可靠、低品质内容。依版权协议,译文需在编辑摘要注明来源,或于讨论页顶部标记{{Translated page}}标签。 此條目翻譯品質不佳。 (2021年10月28日)翻譯者可能不熟悉中文或原文語言,也可能使用了機器翻譯。請協助翻...

 

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!