Wakarmeli
Nembo ya shirika.
Bikira Maria wa Mlima Karmeli na Wakarmeli watakatifu (Simon Stock (amesimama), Anjelo wa Yerusalemu (amepiga magoti), Maria Magdalena wa Pazzi , Teresa wa Yesu ). Picha hii ya Pietro Novelli (1641 ) inatunzwa kwenye "Museo Diocesano", Palermo , Italia .
Sista mmonaki Mkarmeli akijisomea chumbani .
Wakarmeli (kwa Kilatini Ordo Fratrum Beatissimæ Virginis Mariæ de Monte Carmelo , kwa Kiingereza Order of the Brothers of the Blessed Virgin Mary of Mount Carmel , kifupi O.Carm. ) ni watawa wa Kanisa Katoliki ambao labda ulianzishwa katika karne ya 12 kwenye mlima Karmeli (Israeli ) ukizingatia juhudi za nabii Elia zilizojumlishwa katika maneno yake yanayotumika kama kaulimbiu ya shirika: "Zelo zelatus sum pro Domino Deo exercituum" (yaani "Nimefanya bidii sana kwa Bwana Mungu wa majeshi"). Pia kuna uhusiano wa pekee na Bikira Maria .
Mbali ya wanaume , wapo wanawake wamonaki wanaojifungia katika ugo wa monasteri , na masista wenye utume wa aina mbalimbali. Hatimaye wapo walei wanaofuata karama ya shirika ambayo ni hasa kuzama katika sala .
Walio wengi wanafuata urekebisho wa Wakarmeli Peku (kwa Kilatini "Ordo Carmelitarum Discalceatorum", kwa kifupi "O.C.D."), ulioanzishwa na Teresa wa Yesu katika karne ya 16 huko Hispania .
Watakatifu Wakarmeli
Alberto wa Yerusalemu , askofu
Alberto wa Sicilia , padri
Andrea Corsini , askofu
Anjelo wa Sicilia , padrí
Avertano
Brocardo , padri
Elia Kuriakose Chavara , padri
Elizabeti wa Utatu , bikira
Joaquina Vedruna
Maria Magdalena wa Pazzi , bikira
Nuño Alvares de Pereira
Petro Tomas , askofu
Rafael Kalinowski , padri
Simon Stock , presbítero
Teresa Benedikta wa Msalaba (Edith Stein ), bikira
Teresa Margarita Redi , bikira
Teresa wa Yesu , bikira, mwalimu wa Kanisa
Teresa wa Mtoto Yesu , bikira, mwalimu wa Kanisa
Yohane wa Msalaba , padri, mwalimu wa Kanisa
Wenye heri Wakarmeli
Ana wa Mt. Bartolomeo , bikira
María Lopez Rivas , bikira
Arcangela Girlani , bikira
María wa Umwilisho , religiosa
Angelo Agostino Mazinghi , presbítero
Maria wa Yesu Msulubiwa , bikira
Maria wa Malaika , bikira
Luis Rabata , padri
Wafiadini wa Guadalajara , mabikira
Bartolomeo Fanti , padri
Baptista Mantuano , padri
Dionisio wa Noeli , mfiadini
Redento wa Msalaba , mfiadini
Romeo wa Lucca
Enrique wa Osso , padri
Franciska wa Amboise
Francisko Palau , padri
Franco wa Siena
Teresa María wa Msalaba , bikira
Jacobino de Canepacis
Teresa wa Los Andes , bikira
Teresa wa Mt. Augustino na wenzake, mabikira na wafiadini
Tito Brandsma , padri mfiadini
Yoana Scopelli , bikira
Yoana wa Tolosa , bikira
Yohane Soreth , padri
Marejeo
Schaff-Herzog Encyclopedia of Religion
Copsey, Richard and Fitzgerald-Lombard, Patrick (eds.), Carmel in Britain: studies on the early history of the Carmelite Order (1992–2004).
"The Carmelite Order" by Benedict Zimmerman. The Catholic Encyclopedia , 1908.
T. Brandsma, Carmelite Mysticism, Historical Sketches: 50th Anniversary Edition , (Darien, IL, 1986), ASIN B002HFBEZG
J. Boyce, Carmelite Liturgy and Spiritual Identity. The Choir Books of Kraków , Turnhout, 2009, Brepols Publishers, ISBN 978-2-503-51714-8
W. McGreal, At the Fountain of Elijah: The Carmelite Tradition , (Maryknoll, NY, 1999), ISBN 1-57075-292-3
J. Smet, The Carmelites: A History of the Brothers of Our Lady of Mt. Carmel , 4. vol. (Darien IL, 1975)
J. Welch, The Carmelite Way: An Ancient Path for Today’s Pilgrim , (New York: 1996), ISBN 0-8091-3652-X
Viungo vya nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu . Je, unajua kitu kuhusu Wakarmeli kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .