Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake. Hivyo mwaka1982jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita vifupi vya wiki 6 Argentina ilishindwa; takriban wanajeshi 1,000 waliuawa.
Jiografia
Funguvisiwa lina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban km² 6,000. Mwinuko mkubwa ni mlima Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) wenye kimo cha mita 708 juu ya uwiano wa bahari.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Falkland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!