Verdiana wa Castelfiorentino (pia: Viridiana Attavanti; 1182 - 1242) alikuwa bikira aliyepokewa na Fransisko wa Asizi katika Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko ambaye tangu ujanani hadi uzeeni aliishi kama mkaapweke akiwa amejifungia ndani[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Klementi VII mwaka 1533.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Februari[2].