Universities' Mission to Central Africa, kwa kifupi "UMCA", (1857 - 1965) ilikuwa jumuiya ya wasomi iliyoanzishwa na wanachama wa Kanisa la Anglikana katika vyuo vikuu vya Oxford, Cambridge, Durham na Dublin.
Kutokana na wito wa mmisionari David Livingstone, jumuiya hii ilianzishwa katika ya Waanglikana wenye mwelekeo wa Kikatoliki, nayo iliunda vituo vya uaskofu huko Zanzibar na Nyasaland (baadaye Malawi) na kuanzisha mafunzo ya wachungaji wa Kiafrika.