Uasi wa Mabondia (kwa Kiingereza: Boxer Rebellion) ulikuwa tukio kubwa la China miaka 1900 na 1901, ambapo kundi la wazalendo lilitumia nguvu ili kufuta athari ya kigeni nchini mwao.
Wageni nchini China
Wakati huo nchi nyingi za nje zilikuwa zikitawala sehemu za China, zikiwemo hasa Japani, Ufalme wa Muungano, Ujerumani na Russia. China ilikuwa imeshindwa nazo mara nyingi ikawa inadhalilishwa.
Mabondia
Walioitwa na Wazungu "Boxers", yaani "Mabondia", walikuwa raia wa China waliochukia hali hiyo na kwa sababu hiyo walitaka kupigania uhuru kamili kwa kufukuza wageni wote na hata baadhi ya Wachina wenzao. Jina lilitokana na sanaa ya mapigano iliyotumiwa na wazalendo. Waliungwa mkono na wananchi wengi wakapigana hadi Beijing. Kati ya waliouawa nao kuna wamisionari 200 na Wakristo wenyeji 32,000.
Walipigana siku 55, lakini hatimaye wakashindwa. Wageni walifanya sherehe, wakazungukazunguka wakiiba mali ya wenyeji na kubakawanawake. Jemadari wao alikasirika lakini alishindwa kuwazuia.
Matokeo
Washindi walidai Wachina pesa na maeneo mengine pamoja na uuaji wa Mabondia wote.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uasi wa Mabondia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!