Theodosia wa Konstantinopoli (karne ya 7 - 729) alikuwa mwanamke mmonaki wa Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, aliyeuawa chini ya kaisari Leo III wa Bizanti kwa sababu ya kulinda na wenzake picha takatifu ya Kristo isiharibiwe[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Julai[2] au 29 Mei.