Tendi ni tungo ndefu za ushairi zinazoelezea juu ya matukio ya kishujaa yaliyofanywa na watu fulanifulani.
Tendi hazina tofauti kubwa na tenzi, isipokuwa zenyewe hukazia zaidi juu ya matukio ya kishujaa, wakati tenzi hukazia jambo lolote.
Mfano wa tendi ni:
MWOKOZI AJA
1. Mimi kwako ni baba,
Napenda ujitukuze,
Maana umefanikiwa,
Uemshinda yule mwovu,
Imani kuipokea,
Kwa nguvu umemwangusha.
2. Kumbuka umepigana,
Sio kwa mambo ya dunia,
Ushindi umeuleta,
Watoto washangilia,
Amani umawaletea,
Kwa mto umemwangamiza,
Adui yetu mwovu.