Suksesi, Paulo na Lusio (walifariki 250 hivi) walikuwa maaskofu Wakristo ambao, baada ya kushiriki mtaguso mjini Karthago (Tunisia) waliuawa katika dhuluma ya kaisari Decius [1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 18 Januari[2].