Sherman Alexander Hemsley (1 Februari, 1938 – 24 Julai, 2012) alikuwa mwigizaji Mmarekani aliyejulikana zaidi kama George Jefferson katika mifululizo ya CBS All in the Family na The Jeffersons, na kama mhudumu Ernest Frye katika mfululizo wa NBS Amen. Yeye aliigiza pia bosi wa kuogofya wa Earl Sinclair, triseratopsi aliyepewa jina B.P. Richfield, kwenye tamthilia ya futuhi ya Jim Henson Dinosaurs.