Alipokuwa mtoto alikimbia 1966 kwenda Uingereza kwa sababu waziri mkuuMilton Obote alimpindua rais wa Uganda aliyekuwa baba yake Kabaka Mutesa II. Ronald alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Cambridge (Uingereza).
Mwaka 1986 alirudi Uganda. Baada ya kuelewana na serikali ya rais Yoweri Museveni alitawazwa 1993 kama kabaka wa 36 wa Buganda.