Haki ya chakula ,ni Haki ya binadamu inayolinda Haki ya watu kujilisha wenyewe kwa heshima, ikimaanisha kuwa chakula Cha kutosha kinapatikana,kwamba watu wananjia za kukipata na kinakidhi mahitaji ya lishe ya mtu binafsi.Haki ya chakula hulinda Haki ya binadamu kwa Uhuru kutokana na njaa,uhaba wa chakula na utapiamlo.[1]Haki ya chakula aimaanishi kwamba Serikali ina wajibu wa kusambaza chakula kwa Kila mtu anayeitaji au Haki ya Kulishwa.Hata hivyo ikiwa watu wanashindwa kupata chakula kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao kwa mfano Hali ya Vita au baada ya majanga ya asili haki inahitaji Serikali kutoa chakula Moja kwa moja.[2]
Marejeo