Baada ya kupadirishwa mwaka 1242 akiwa na miaka 45, akarudi Uingereza na kufanya kazi ya paroko Charing na Deal (mkoa wa Kent), lakini akarejeshwa mapema katika ukatibu mkuu.
Askofu
Mwaka 1244 alichaguliwa na maaskofu kuongoza jimbo la Chichester, lakini mfalmeHenry II alimtaka Richard Passelewe, hivyo akazuia mali na mapato ya jimbo.
Askofu mpya aliporudi Chichester, alilazimika kuishi kifukara katika nyumba ya paroko wa Tarring (Sussex), akifanya kazi za mikono na kutembelea jimbo lote kwa miguu. Miaka miwili baadaye mfalme Henry III alilazimishwa na Papa kulirudishia jimbo mali zote.
Matendo ya upendo
Richard alikuwa mkarimu sana kwa fukara na mpole kwa wakosefu. Alitunga sheria za jimbo, ambazo zinadumu hadi leo, kuhusu masuala mbalimbali.
Kifo
Akiwa Dover ili kumjengea kanisa hayati mwalimu wake Edmund Rich, aliugua sana akafa tarehe 3 Aprili 1253.
Sala yake
Asante kwako, Bwana wangu Yesu Kristo, kwa fadhili zote ulizonistahilia.
Kwa mateso na matusi yote uliyoyavumilia kwa ajili yangu.
Mkombozi, rafiki na kaka mwenye huruma nyingi,
naomba niweze kukufahamu wazi zaidi, kukupenda kwa hisani zaidi,
kukufuata kwa karibu zaidi, siku kwa siku.
Diana E. Greenway (1996). "Bishops". Fasti Ecclesiae Anglicanae 1066-1300: volume 5: Chichester. Institute of Historical Research. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-08. Iliwekwa mnamo 21 Oktoba 2007.
Bullock-Webster, G.R. (1913). The Churchman's Prayer Manual. London: Published by Author.
Butler, Alban. Lives of the Saints. Tan Books and Publishers: Rockford, 1955
Farmer, David Hugh (2003). "The Oxford Dictionary of Saints". Oxford University Press. Oxford Reference Online. Oxford University Press. West Sussex County Library Service. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2011. -subscription required.
Foster, Paul, mhr. (2009). Richard of Chichester (1197 - 1253). Chichester: University of Chichester. ISBN978-0-948765-42-1.
Fryde, E. B. (1996). Handbook of British Chronology (tol. la Third Edition, revised). Cambridge: Cambridge University Press. ISBN0-521-56350-X. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
Headlam, Cecil (1898). Prayers of Saints :Being A Manual of Devotions Compiled from the Supplications of the Holy Saints and Blessed Martyrs and Famous Men. London: F.E. Robinson.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.