Polieni, Serapioni na Justili ni kati ya Wakristo wa Misri waliouawa kwa ajili ya imani yao.
Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yao, hawaorodheshwi tena na Martyrologium Romanum.
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Agosti.