Milima ya Udzungwa

Milima ya Udzungwa.
Mlima ya Udzungwa

Milima ya Udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana katika bara la Afrika, nchini Tanzania, hasa mkoani Iringa, Wilaya ya Kilolo, na kidogo mkoa wa Morogoro, wilaya ya Kilombero.

Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi.

Jina la hifadhi limetokana na milima hiyo ya Udzungwa (yaani nchi ya Wadzungwa, tawi la Wahehe). Kilele cha juu ni Mlima Luhombero (Iringa) (mita 2,579).

Ina ukubwa wa kilometa mraba 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani.

Maporomoko ya Sanje

Kati ya aina kumi na moja za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni: "Mbega Mwekundu wa Iringa" (Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka 1979. Kuna aina nyingine nne za ndege ambao hawakufanyiwa uchunguzi ambao ni: chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya iliyogunduliwa ya aina ya kwale wa Udzungwa zinazofanya hifadhi hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika.

Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, chui, nyati na tembo.

"African violet" ni ua ambalo linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya miti mirefu inayofikia mita 30.

Pia Mto Sanje ni kivutio kikubwa sana. Mto huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!