Masedoni, Teoduli na Tasiani (walifariki Meros, Frigia, leo nchini Uturuki, 362 hivi) walikuwa Wakristo ambao kwa amri ya gavana Almaki, baada ya kuteswa kikatili, walichomwa moto kwa kubanikwa kwa ajili ya imani yao katika dhuluma ya kaisari Juliani Mwasi[1].
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao ni tarehe 19 Julai[2] au 12 Septemba au 13 Septemba.