Marc Batchelor (4 Januari 1970 - 15 Julai 2019) alikuwa mchezaji wa soka wa Afrika Kusini ambaye alicheza kama mshambuliaji.
Batchelor alijiunga na timu mbalimbali nchini Afrika kusini ikiwemo Wanderers, Balfour Park, Berea Park, Defence na Dynamos mwaka 1990.[1][2] Baadaye alicheza katika klabu ya Bidvest Wits F.C, Orlando Pirates, SuperSport United, Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na Moroka Swallows. Alishinda mataji manne makubwa akiwa na klabu ya Orlando Pirates ikijumuisha Kombe la Mabingwa wa Afrika la mwaka 1995.[3] Baada ya kustaafu kwenye soka la kulipwa mwaka 2003 alifanya kazi kama mchambuzi wa mpira wa televisheni. Hata hivyo, alifutwa kazi mwaka 2007 baada ya kupigana katika mgahawa Mwaka 2014 Batchelor alikuwa shahidi katika kesi ya Oscar Pistorius.[4] Aliuwawa nje ya nyumbani kwake huko Olivedale tarehe 15 Julai 2019.[1][3][5][6]
{{cite journal}}
|dead-url=
|url-status=