Maksimiliani wa Tebessa (au Numidia; 274- 12 Machi 295) alikuwa kijana Mkristo katika Algeria ya leo aliyefia dini yake kwa kukatwa kichwa[1].
Mtoto wa askari Fabius Victor, alilazimishwa kujunga na jeshi la Dola la Roma, lakini alikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Kaisari na kuwa mwanajeshi akitaja kama sababu imani yake[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Machi[3].