Klaudi, Asteri na Neoni (walifariki Egea, 303 ) walikuwa ndugu Wakristo wa Kilikia, leo nchini Uturuki, waliofia dini yao kwa kukatwa kichwa chini ya gavana Lisia wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].
Tangu kale wote wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama watakatifu[2].
Sikukuu yao ni tarehe 23 Agosti[3].