Picha mbili za Kamchatka kutoka angani; kushoto: rasi wakati wa Juni, kuna mawingu mengi upande wa mashariki; kulia: rasi yote pamoja na bahari ya karibu imefunikwa kwa theluji na barafu wakati wa Januari.
Rasi ya Kamchatka (rus.полуо́стров Камча́ткаpoluostrov Kamchatka) ni rasi kwenye upande wa wa mashariki ya Urusi. Ina urefu wa kilomita 1,250 na eneo la 270,000 km².[1]
Kiutawala ni sehemu ya mkoa wa Kamchatka Krai mwenye wakazi 322,079. Zaidi ya nusu ya wakazi hawa wanaishi katika miji miwili ya Petropavlovsk-Kamchatsky (waakzi 179,526) na Yelizovo (38,980).
Marejeo
↑Быкасов В. Е.Ошибка в географии // Известия Всесоюзного Географического Общества. — 1991. — № 6. (Kirusi)