'Jana Sio Leo ni wimbo wa Zola D akimshirikisha Dknob na Mez B. Wimbo ulitayarishwa katika studio ya Mandugu Digital ya Dar es Salaam, ikiwa chini ya utayarishaji wake Shark na Back Stage kunako mwaka wa 2003. Wimbo umepata kushika chati kadhaa katika maredio ya Dar - sanasana katika Times Fm redio.
Waliouza sura katika video ya jana sio leo alikuwa Mr. Dude, Mtanga na wengineo kibao. Video yake ilifanywa na kampuni utengenezaji wa filamu na video za muziki iitwayo Rav Production. Vilevile nyimbo hii imepata kuwa kama kibwagizo cha filamu ya Nyuma ya Pazia ya mwaka 2003.
Tazama pia
Viungo vya nje
|
---|
Albamu zake | |
---|
Single zake | |
---|
Single zingine | |
---|
Makala zinazohusiana | |
---|