Felisi wa Afrika Kaskazini (alifariki baada ya 453) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki.
Alipelekwa uhamishoni katika dhuluma ya Genseriki, mfalme wa Wavandali.
Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Novemba[1].