Enda wa Aran (pia: Éanna, Éinne au Endeus; Meath, 450 hivi – Killeaney, 530 hivi) alikuwa mtemi na askari katika nchi ya Ireland ambaye, kwa shauri la dada yake, Fanchea, akawa mmonaki na padri .
Anatajwa kama baba wa umonaki wa Ireland kwa sababu alianzisha monasteri mbalimbali, hasa ile maarufu ya Aran, hivi kwamba watakatifu wengi walihusiana nazo[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 21 Machi[2].