Dioskoro mfiadini ni kati ya Wakristo wa Misri waliouawa kwa ajili ya imani yao.
Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Agosti.