Guevara kwa sababu ya kufiwa na bibi yake aliyemuuguza kwa muda mrefu aliamua kusomea utabibu.
Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umaskini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi, huku wachache wakiwa wanamiliki mali za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa umaskini na ukandamizaji ni mapinduzi. Aliamua kusoma kwa undani falsafa ya Karl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za kisoshalisti nchini Guatemala chini ya raisJacobo Arbenzi Guzmán.
Mwisho mwa miaka ya 1950, Guevara aliungana na Fidel Castro aliyekuwa akiongoza kundi la kijeshi lililotwaa madaraka kwa nguvu nchini Kuba mwaka 1959. Guevara alikuwa mmoja wa viongozi wa serikali mpya ya Kuba. Katika kipindi hiki, Guevara aliandika vitabu na makala mbalimbali kuhusu nadharia na vitendo vya vita vya msituni kwa nia ya kuondoa madarakani tawala za kibepari na kibeberu.
Guevara aliondoka nchini Congo na kuelekea Bolivia ambapo alikamatwa mwaka 1967 na jeshi la Bolivia likishirikiana na majasusi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA). Jeshi lilitangaza kutoa zawadi nono kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa Che Guevara. Baada ya kukamatwa kwake, aliuawa kinyama.
Baada ya kifo chake, Guevara alichukuliwa kama nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina ya Beret aliyopenda kuivaa, vimekuwa kama alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto duniani.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Che Guevara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!