Tangu mwaka 2010 kundi hilo linatumia jina rasmi la جماعة أهل السنة للدعوة والجهاد, jamāʿat ahl as-sunna li-d-daʿwa wa-l-ǧihād, yaani "jumuiya ya watu wa Sunna kwa ajili ya uenezaji (wa Uislamu) na jihadi".
[4]
Imekadiriwa ya kwamba mapigano yaliyoanzishwa na Boko Haram au kutekelezwa dhidi yake yamesababisha vifo vingi, Rais wa Nigeria Jonathan Goodluck alidai Mei 2014 kuwa kundi lilisababisha vifo vya watu 12,000 na wajeruhiwa kwa maisha 8,000.
[5][6][7][8][9][10][11]
Baada ya kushambulia shule, vituo vya polisi,makanisa na ofisi za serikali kundi lilitoa tamko mwaka 2012 kuwa linawapa Wakristo wote nafasi ya siku 3 kuondoka kaskazini mwa Nigeria au watauawa. Tangu tangazo lile mashambulio yameongezeka. Hawashambulii Wakristo na mapolisi pekee lakini pia idadi kubwa ya Waislamu ambao ndio wakazi wengi kaskazini.
Mnamo Aprili 2014 kundi la Boko Haram likashambulia mji wa Chibok katika jimbo la Borno, likaweka moto na kuharibu nyumba 170 na kuingia shule ya sekondari walipokamata wasichana zaidi ya 200, Tarehe 6 Mei 2014, wasichana wengine 8 walitekwa na watu wenye silaha wanaofikiriwa kuwa wa kundi hilohilo.[12][13]
Kiongozi wa Boko Haram, Shekau alitisha kuwauza mabinti kama watumwa[14].
Tarehe 12 Mei 2014 video ya Boko Haram ilidai kuwa mabinti wote waweongokea Uislamu na watashikwa hadi wafungwa wa Boko Haram waliomo mkononi mwa serikali watakapoachishwa na kuwekwa huru. .[15]
↑Olugbode, Michael. "Nigeria: We Are Responsible for Borno Killings, Says Boko Haram", All Africa, 2 February 2011. Retrieved on 31 January 2012. "The sect in posters written in Hausa and pasted across the length and breadth of Maiduguri Wednesday morning signed by the Warriors of Jamaatu Ahlis Sunna Liddaawati Wal Jihad led by Imam Abu Muhammed Abubakar Bi Muhammed a.k.a. Shehu claimed they embarked on the killings in Borno ‘in an effort to establish Sharia system of government in the country’."