Bafu

Bafu ya kisasa iliyo na choo.

Bafu (pia maliwato) ni chumba kilichotengwa cha kuogea ambacho walau huwa na beseni au karai la kuogea. Huenda bafu ikawa ndani ya nyumba kunakokaa watu au hata nje kando ya nyumba ile. Katika nyumba za kisasa, bafu huambatanishwa na choo. Katika jamii ya Kiamerika, neno bafu huashiria mahala pa kukogea na pia kutabawali. Kwa hivyo, mabafu yao huwa na choo ndani.

Neno hili, pamoja na neno hamamu, linaweza kutaja pia jengo lenye beseni kubwa la kuogelea kwa umma wa watu wengi au watu kuoga. Kihistoria kuwepo kwa bafu au hamamu za kijamii kulikuwa taasisi muhimu kwa afya ya umma. Katika mazingira ambako teknolojia haikuwa bado na uwezo ya kupeleka maji na nishati katika kila nyumba, bafu au hamamu za umma ziliwapa watu wengi nafasi ya kujisafisha na hivyo kupunguza nafasi za kusambaa kwa magonjwa yanayotegemea uchafu.

Historia ya bafu

Katika historia za jamii nyingi, kukoga hakukufanywa na mtu akiwa peke yake. Watu walioga wakiwa pamoja. Hata leo, tendo la kukoga kwa pamoja bado lafanywa katika nchi kama Japani na Uturuki ambako bafu huwa kubwa na watu huingia kukoga wote pamoja. Bafu la kwanzal ilionekana miaka ya 3000 kabla ya ujio wa Yesu Kristo.

Bafu lilikuwa na umuhimu sana katika dini maana ukienda kukoga, ilikuwa na maana kwamba umeoga mwili na pia roho yako kwa ndani .

Vifaa vya bafuni

Ndani ya bafu utapata taulo ya kujipangusia baada ya kukoga. Pia utapata sabuni ya kuogea, mafuta ya kujipaka na pia katika mabafu mengine kuna pahala pa kuning'iniza nguo za ndani ili zikauke baada ya kuzifua.

Kuna beseni au karai la kuogea, mifereji ya maji. Mabafu ya leo huwa na mfereji ulio juu, hivi kwamba mtu anaweza kuoga kwa maji yanayunyuka kutoka juu.

Bafu pia huwa na stima ili kwamba uweze kutumia maji moto unapokoga.

Shawa za juu na zinazobebwa

Hivi majuzi, kumekuwa na mifereji inayokuwa juu hivi kwamba unapokoga, maji yatiririka kutoka juu. Shawa nyingi kama hizi hutumia kawi ya stima.

Kwa wanaopenda kukita kambi maeneo mbali mbali, kuna shawa zinazoweza kubebwa kutoka mahali pamoja hadi kwingine

Samani katika bafu

Bafu za kisasa huwa na samani kama vile kabineti za kuwekea vitu vya kukoga, nyembe za kunyoa nywele pamoja na dawa. Utapata kuwa kuna rafu za kuwekea tauli baada ya kuzifunga vizuri. Kuna nyinginezo zenye wadirobu ya kuwekea nguo.

Shawa ya bideti kwa Waislamu

Bafu za Waislamu huwa na kifereji kinachoitwa bideti ambacho humwezesha Mwislamu kukoga na kusafisha makalio baada ya kutumia choo kwa haja kubwa. Bideti ni kifereji hiki ambacho huweza kushikwa kwa mkono kama tu kile kinyunyizi cha jikoni cha kusafisha vyombo. Bideti hii hushikwa kwa mkono na kuelekezwa kwa makalio haswa mtu asipotumia kijikaratasi chepesi (tishu) kujifutia. Bafu zilizo na bideti zimeshamiri katika mataifa kama Misri, Uchina, Pakistani, Uarabuni, Malaysia na Vietinamu.

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bafu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.