Aleksanda wa Lyon (alifariki Lyon, mji mkuu wa Gallia, leo nchini Ufaransa, 24 Aprili 178) alikuwa tabibu Mkristo kutoka Frigia, Uturuki, ambaye, baada ya mateso makali, alisulubiwa katika dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo iliyosababisha mauaji makubwa katika mji wa Lyon [1][2].
Ilikuwa siku mbili baada ya rafiki yake mkuu, Epipodi, kukatwa kichwa kwa ajili ya imani.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[3][4].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[5].