"When You Say Nothing at All" ni wimbo wa mwenendo wa country uliotungwa na by Paul Overstreet na Don Schlitz. Ni mmoja wa zile nyimbo ambazo zinajulikana kuvuma zaidi kwa wasanii watatu: Keith Whitley, ambaye aliuchukua uongzini mwa chati za BillboardHot Country Singles mnamo 24 Desemba 1988; Alison Krauss, ambaye toleo lake lilikuwa lake la kwanza la solo katika kumi bora za mwenendo wa country zilizovuma mnamo 1995; na mwimbaji wa IrelandRonan Keanting ambaye toleo lake lilikuwa solo yake ya kwanza na liliongoza chati za UK.
Kiini
Overstreet na Schlitz waliubuni wimbo huu mwishoni mwa siku ambayo haikuwa na mapato mengi. Huku wakipiga gitaa na kujaribu kufikiria wimbo wao ambao ungefuatia. Hawangeweza kufikiria kitu. “Wakati tukijaibu kutafuta njia nyingine ya kutosema kitu, tuliubuni wimbo huu,” ," Overstreet alimwambia mhariri Ace Collins baadaye. Walionelea wimbo ulikuwa sawa lakini haukuwa spesheli. .[1]
Wakati Keith Whitley aliusikia wimbo huo, aliupenda na asingeuachilia umpite kamwe[1]. Awali alikuwa ameutayarisha imbo mwingine wa utunzi wa Overstreet-Schlitz ambao ulifika #1 lakini kwa msanii mwingine Randy Travis, wimbo wa "On the Other Hand." Whitley hakuwa tayari kuacha hali hiyo itokee tena kwa wimbo huu.[1][2].
Matoleo
Keith Whitley
RCA ilitoa wimbo huu kama single ya kufuatilia kwa wimbo mkuu wa albamu ya Whitley Don't Close Your Eyes. Wimbo wa awali tayari ulikuwa umevuma katika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot Country Singles, wimbo wake wa kwanza kuongoza katika chati hizo[3].
"When You Say Nothing at All" uliingia katika chati za Hot Country Singles mnamo 17 Septemba 1988 katika nafasi ya 61 na polepole ukanawili kufikia uongozini ambapo ulikaa ka majuma mawili mwishoni mwa mwaka[1][2].
Ulikuwa wa pili katika tano za singles za Whitley (ambaye hakuishi kuona mbili za mwisho) zilizoongoza mtawalia katika chati hizo. Whitley aliaga dunia mnamo 9 Mei 1989 kutokana na umu katika pombe[3].
Mnamo 2004, wimbo wa asili wa Whitley uliorodheshwa wa 12 kati ya nyimbo 100 bora aidi za kimapenzi na CMT[4]. Uliimbwa na Sara Evans katika tamasha hizo.
Alison Krauss
Krauss ambaye alikuwa amekomaa katika muziki wa bluegrass akicheza fiddle katika umri wa miaka 22 aliutoa wimbo wa "When You Say Nothing at All" pamoja na kundi lake ‘’Union Station’’ kama rizala za rambirambi kwa Whitley mnamo 1994. Wakati wimbo huo ulianza kupokea umaarufu, BNA Records, leb ambayo iliutayarisha albamu hiyo ilitoa toleo la Krauss kwa redio mnamo Januari 1995.[5]. toleo hili pia lilishirikishwa katika mkusanyiko wa Krauss Now That I've Found You: A Collection, ambao ulifikia kileleni katika nafasi ya tatu kwa chati za ‘’Billboard’’ Hot Country Singles & Tracks na single ya kuuza ilifikia #2 kwa chati ya Billboard Hot Country Singles Sales. .[3], Uongozi wake na wa albamu nyingine ulimshangaza Krauss ambaye hakuwa akitarajia[6].
Toleo la Krauss lilishinda tuzo la 1995 la CMA kwa "Single bora ya mwaka".
"When You Say Nothing at All" ndiyo ilikuwa single ya kwanza ya solo kwa Ronan Keating baada ya kuliacha kundi la Boyzone. Aliitayarisha mnamo 1999 kama soundtrack ya filamu ya Notting Hill. Wimbo huu pia ungeonekana katika albamu ya kwanza ya solo ya Keating Ronan mwaka uliofuatia.
Toleo la Keating lilitolewa kama single baadaye 1999 na ilifika #1 katika chati za UK. Pia ilifika #1 katika taifa la Ireland. Nchini UK, Single hii ilidhibitishwa kuwa katika kiwango cha ‘’Dhahabu’’ katika mauzo yake.
Mnamo 2002 aliitayarisha single hiyo tena kwa ushirikiano na mwimbaji wa Italia mwenye asili ya BrazilDeborah Blando.
Mnamo 2003 aliitayarisha single hiyo tena wakati huu akishirikiana na mwimbaji wa MexicoPaulina Rubio ambayo waliitoa jijini Mexico na Latin America kama njia ya kukuza albamu ya "Destination".
↑Horak, Terri. "Rounder Goes All Out for Grammy-Nominated Krauss", Billboard, 1995-01-21. Accessed via ProQuest.
↑Cromelin, Richard. "A Hit from Country's Kinfolk / Bluegrass's most prominent figure makes her way into country music's Top 10. Even Alison Krauss can't explain it.", Los Angeles Times, 1995-03-25, p. F1. Accessed via ProQuest.