Walter wa Pontoise

Mt. Walter katika dirisha la kioo cha rangi.

Walter wa Pontoise, O.S.B. (pia: Gautier, Gaultier, Gaucher, Gualtierus; Andainville, Picardie, 1030 hivi [1] – Pontoise, Ijumaa Kuu 1099 hivi) alikuwa mmonaki padri wa Utawa wa Mt. Benedikto nchini Ufaransa, ambaye alikubali kuweka pembeni hamu yake ya kuishi upwekeni akaongoza kama abati wa kwanza monasteri karibu na Paris akitoa mfano wake katika kushika kanuni pamoja na kupinga usimoni wa waklero hata akashindana na mfalme Filipo I wa Ufaransa[2].

Mwaka 1094 alianzisha monasteri ya kike.

Alitangazwa mtakatifu na askofu mkuu Hugo wa Rouen mwaka 1153, wa mwisho kutangazwa na mtu asiye Papa katika Kanisa la Magharibi[3][4] “The last case of canonization by a metropolitan is said to have been that of St. Gaultier, or Gaucher, abbat [sic] of Pontoise, by the Archbishop of Rouen, A.D. 1153. A decree of Pope Alexander III, A.D. 1170, gave the prerogative to the pope thenceforth, so far as the Western Church was concerned.”[3].

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 23 Machi[5].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!