Wakristo 19 maarufu kama Wafiadini wa Gorkum
Wafiadini wa Gorkum (walifariki Brielle , Uholanzi , 9 Julai 1572 , ni Wakristo 19 wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini kwa kuwa walidhihakiwa na kuteswa kikatili wakauawa na Waprotestanti kwa kunyongwa kwa sababu walitetea imani sahihi katika ekaristi na kukataa kujitenga na Papa .
Karibu wote walikuwa mapadri , kumi na mmoja wa kwanza walikuwa Wafransisko , wengine wa mashirika mengine au wanajimbo . Mbali ya Waholanzi, wawili waliotokea Denmark na Ujerumani [ 1] .
Majina yao ni:
Nikola Pieck , padri wa Ndugu Wadogo
Petro wa Assche , bruda wa Ndugu Wadogo
Wilehadi wa Denmark , padri wa Ndugu Wadogo
Teodoriko van der Eem , padri wa Ndugu Wadogo
Nikasi wa Heeze , padri wa Ndugu Wadogo
Antoni wa Hoornaert , padri wa Ndugu Wadogo
Godefrid wa Melveren , padri wa Ndugu Wadogo
Fransisko wa Roye , padri wa Ndugu Wadogo
Antoni wa Weert , padri wa Ndugu Wadogo
Jeromu wa Weert , padri wa Ndugu Wadogo
Korneli wa Wijk-bij-Durstede , bruda wa Ndugu Wadogo
Yohane wa Oisterwijk , padri wa Wakanoni Waaugustino
Yohane Heer , padri wa Wadominiko
Adriani wa Hilvarenbeek , padri wa Wakanoni Wapremontree
Yakobo Lacops , padri wa Wakanoni Wapremontree
Leonardi Veghel , padri mwanajimbo
Nikola Poppel , padri mwanajimbo
Godefrid Duynen , padri mwanajimbo
Andrea Wouters , padri mwanajimbo
Kwanza walitangazwa na Papa Klement X kuwa wenye heri tarehe 24 Novemba 1675 , halafu
watakatifu na Papa Pius IX tarehe 29 Juni 1867 .
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai [ 2] .
Tanbihi
Makala hii bado ni mbegu . Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari .