Wafiadini saba wa Efeso

Mchoro mdogo wa karne XIV ukionyesha Wafiadini saba.

Wafiadini saba wa Efeso (walifia dini Efeso, leo nchini Uturuki, 250 hivi) walikuwa Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[1].

Waliitwa majina haya lakini pia mengine mengi:

  • Konstantino
  • Denisi
  • Yohane
  • Masimiani
  • Malko
  • Machano
  • Serapioni

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 27 Julai[2], au 4 Agosti au 22 Oktoba.

Wanatajwa pia na Kurani, sura ya 18, kwa jina la "Watu wa Pango" (اصحاب الکهف, aṣḥāb al kahf) na katika maandishi mengine.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.